Rudi Nyumbani

Masharti na Vigezo

Ilisasishwa Mwisho: Mei 25, 2026

1. Kukubali Masharti

Karibu sana Studio. Kwa kutembelea, kujisajili, au kutumia huduma za Studio ("Kampuni", "sisi", au "yetu"), unakubali kufuata na kufungwa na Masharti na Vigezo hivi. Ikiwa hukubaliani na miongozo hii, tunakuomba ndugu usitumie huduma zetu. Tuna haki ya kuboresha au kubadilisha masharti haya wakati wowote ili kuendana na ukuaji wa huduma yetu.

2. Maelezo ya Huduma

Studio inatoa huduma za kutengeneza na kuboresha picha kupitia akili mnemba (AI), na huduma nyingine zinazohusiana ("Huduma"). Huduma hii inatolewa "kama ilivyo" na "inavyopatikana". Lengo letu ni kutoa huduma bora, lakini hatuhakikishii kuwa huduma haitakuwa na hitilafu, usumbufu, au makosa ya kiufundi wakati wote.

3. Maadili na Matumizi Sahihi

Ili kulinda jamii yetu na ubunifu, unakubali KUTOTUMIA huduma hii kwa:

  • Kutengeneza, kupakia, au kusambaza maudhui yaliyo kinyume cha sheria, kashfa, au yanayovunja kanuni na sheria za nchi na za kimataifa.
  • Kupakia picha au nyaraka ambazo hauna haki miliki nazo (copyright). Unathibitisha kuwa unamiliki au una ruhusa kamili ya kisheria kutumia, kubadilisha, au kusambaza picha zozote unazopakia kwenye mifumo yetu.
  • Kutengeneza picha za ngono, picha za udhalilishaji bila ridhaa, au maudhui yanayowadhuru watoto.
  • Kuvunja haki miliki, haki za faragha, au haki za kiraia za mtu mwingine yeyote.
  • Jaribio lolote la kudukua, kuharibu, au kuingilia mfumo na usalama wa huduma zetu.

Tuna haki ya kusitisha au kufuta akaunti yoyote inayovunja miongozo hii ili kulinda usalama wa watumiaji wengine na hadhi ya huduma yetu.

4. Usimamizi na Uhifadhi wa Data

Tunathamini sana faragha yako na tunatumia mfumo wa kuhifadhi data kwa uchache:

  • Ufutaji wa Moja kwa Moja: Ili kupunguza mrundikano wa data, Studio huhifadhi picha tatu (3) tu za mwisho ulizotengeneza kupitia huduma za wingu (Cloud). Picha za zamani hufutwa moja kwa moja kutoka kwenye seva zetu.
  • Uhifadhi wa Ndani (Local Storage): Baadhi ya zana zetu za uhariri (kama vile Background Removal na Image Compressor) huchakata picha moja kwa moja ndani ya kifaa chako (Browser). Tunatumia teknolojia za kisasa kama IndexedDB kuhifadhi kazi hizi kwa muda kwenye kifaa chako pekee, kuhakikisha faragha yako inalindwa kikamilifu bila kutuma data kwenye mtandao.
  • Udhibiti wa Mtumiaji: Una haki kamili ya kufuta data yako na akaunti yako wakati wowote kwa kudumu kupitia sehemu yako ya mipangilio (dashboard).

5. Ukomo wa Dhima

Kwa kiasi kinachoruhusiwa na sheria, Studio na washirika wake hawatowajibika kwa hasara yoyote ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja inayotokana na matumizi yako ya huduma, ikiwemo upotevu wa data, faida, au sifa, kutokana na matumizi au kushindwa kutumia huduma hii. Kwa vyovyote vile, dhima ya juu zaidi ya Studio kwa madai yoyote yanayotokana na matumizi ya huduma hii haitazidi kiasi ulicholipa kwa huduma katika miezi kumi na mbili (12) iliyopita au $100, kiasi chochote kile kilicho kikubwa zaidi.

6. Fidia

Unakubali kuilinda na kuiepusha Studio, wakurugenzi wake, na wafanyakazi wake dhidi ya madai yoyote, hasara, au gharama (ikiwemo ada za mawakili) zinazotokana na matumizi yako ya huduma au uvunjifu wako wa Masharti haya.

7. Miliki ya Ubunifu

Muonekano, michoro, na msimbo wa huduma hii ni mali ya Studio na washirika wake. Kuhusu picha unazotengeneza: unatupea ruhusa ya kuhifadhi na kutumia maudhui hayo kwa lengo la kuendesha na kuboresha huduma zetu pekee. Kwa sababu tunahifadhi picha tatu tu za mwisho, tafadhali hakikisha unapakua (download) picha zako unazotaka kuzitunza kwa muda mrefu.

8. Mfumo wa Credits na Malipo

Ununuzi wowote wa "Credits" ndani ya Studio ni wa mwisho na haurejeshwi, isipokuwa pale sheria inapoelekeza vinginevyo. Credits hizi hazina thamani ya fedha nje ya mfumo wetu na haziwezi kubadilishwa kuwa pesa taslimu. Mfumo utarejesha credits zako moja kwa moja (Refund) endapo kutatokea hitilafu ya kiufundi kwenye seva zetu inayozuia kukamilika kwa kazi ya AI uliyoomba. Studio haitahusika na upotevu wa credits ikiwa akaunti itafungwa kutokana na uvunjifu wa Masharti haya. Tuna haki ya kusitisha, kufungia akaunti, au kuzima upatikanaji wa API endapo kutabainika ukiukwaji wa Masharti haya, majaribio ya kudukua mifumo ya credits, au kwa sababu muhimu za kiusalama na kiutendaji. Zaidi ya hayo, madai yoyote ya uongo ya kurejesha fedha kupitia benki (Chargebacks) yatasababisha kufungiwa kwa akaunti yako moja kwa moja na kupoteza credits zilizobaki.

9. Umiliki wa Kazi za AI na Haki Miliki

Unamiliki haki zote za picha na maudhui unayotengeneza kupitia huduma yetu. Hata hivyo, kwa kutumia huduma hii, unatupa leseni ya kudumu, ya kimataifa, na ya bure (royalty-free) ya kuhifadhi na kutumia maudhui hayo na maelezo unayoingiza (prompts) kwa lengo la kuendesha na kuboresha mifumo yetu.

10. Sheria Inayoongoza na Usuluhishi

Masharti haya yanasimamiwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Migogoro yoyote itatatuliwa kwa njia ya usuluhishi (Arbitration) wa kisheria badala ya mahakama za kawaida. Kwa kukubali masharti haya, unaachana na haki ya kushiriki katika mashtaka ya jumuia (Class Action Waiver).

11. Sera ya Hakimiliki (DMCA)

Tunaheshimu haki miliki. Ikiwa unaamini kazi yako inatumika kwa njia inayovunja hakimiliki kupitia huduma zetu, tafadhali wasiliana nasi. Tuna haki ya kufuta maudhui yanayolalamikiwa na kufungia akaunti za watumiaji wanaovunja sheria za hakimiliki mara kwa mara.

12. Nguvu ya Asili (Force Majeure)

Studio haitawajibika kwa kuchelewa au kushindwa kutoa huduma kutokana na majanga ya asili, kukatika kwa mtandao mkuu, matatizo ya watoa huduma wetu wa AI, au mazingira mengine yaliyo nje ya uwezo wetu. Endapo kuna kifungu chochote cha masharti haya kitakachoonekana kuwa batili kisheria (Severability), vifungu vilivyobaki vitaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Ikiwa una swali lolote kuhusu Masharti haya, tafadhali wasiliana nasi kupitia info@watulab.com Tunashukuru kwa kuwa sehemu ya familia ya watumiaji wa huduma yetu.
© 2026 Watulab. All rights reserved.
1