Ilisasishwa Mwisho: Mei 25, 2026
Hapa Studio, faragha yako na usalama wako wa kisheria ni mambo tunayoyapa kipaumbele cha juu sana. Sera hii ya Faragha inaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuchakata, na kulinda taarifa zako unapotumia huduma zetu.
Tunatumia data zako kwa uaminifu mkubwa kwa sababu zifuatazo pekee:
Tunasisitiza kuwa HATUUZI kabisa data zako kwa watu au Taasisi za nje.
Taarifa zako hushirikishwa tu na washirika wetu wanaoaminika (kama vile watoa huduma za seva na ujumbe wa OTP) ambao wamefungwa na mikataba mikali ya usiri. Tunaweza kutoa taarifa zako pale tu sheria inapotulazimu kufanya hivyo ili kulinda kampuni yetu au usalama wa watumiaji wengine.
Tunatumia teknolojia ya kisasa ya usimbaji (encryption kama TLS/SSL) na tunaficha nywila zako kwa usalama wa hali ya juu. Ingawa tunajitahidi kwa kila hali kulinda data zako, hakuna mfumo wa mtandaoni ulio salama kwa 100%. Hivyo, unatumia huduma hii kwa ridhaa yako huku ukitambua hatari zinazo weza kujitokeza, tunaendelea kuimarisha usalama wa mifumo yetu kadri ya uwezo wetu wa kibinadamu.
Una haki ya kuona, kusahihisha, au kuomba kufutwa kabisa kwa data zako. Unaweza kufuta picha ulizotengeneza moja kwa moja kwenye dashboard yako. Ikiwa unataka kufuta akaunti yako yote, unaweza kuwasiliana na timu yetu. Mara ombi la kufuta akaunti linapopokelewa, data zako zitafutwa kabisa kwenye mifumo yetu ndani ya siku 3 za kazi (ingawa baadhi ya kumbukumbu za kisheria zinaweza kubaki kwa muda mrefu zaidi kwa ajili ya usalama na kufuata sheria).
Tunaweza kuboresha Sera hii ya Faragha mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia au sheria. Tunakushauri kupitia ukurasa huu mara kwa mara. Mabadiliko yoyote yataanza kufanya kazi mara tu yatakapo fanyiwa marekebisho.
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania (PDPA), unakubali kwamba data zako zinaweza kuhamishwa na kuhifadhiwa kwenye seva zilizo nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huduma zetu hutumia mifumo ya AI ya kampuni za nje (kama vile Google au washirika wengine). Maelezo unayoingiza (prompts) na picha zinazotengenezwa zinaweza kuchakatwa na seva za washirika hawa wa kimataifa. Tunakushauri usijumuishe taarifa zako za siri, za afya, au za utambulisho (PII) unapoomba picha.
Huduma hii haijaundwa na hailengi watoto walio chini ya umri wa miaka 18. Hatukusanyi kwa makusudi taarifa za watoto. Ikiwa tutabaini tumekusanya data za mtoto chini ya umri huo, tutazifuta mara moja.
Ikitokea ukiukwaji mkubwa wa usalama wa data ambao unaweza kuhatarisha haki zako, tutakujulisha wewe pamoja na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania (Tanzania Personal Data Protection Commission) ndani ya saa 72, kulingana na matakwa ya PDPA na viwango vya kisheria vya kimataifa (k.m., GDPR).
Kulingana na eneo lako (kama vile Ulaya kwa GDPR au California kwa CCPA), una haki maalum ikiwemo kuomba nakala ya data zako, kupinga uchakataji wa data, au kuomba data zako zihamishwe (Data Portability). Wasiliana nasi kupitia barua pepe yetu kutekeleza haki hizi.
Tunatumia teknolojia za kisasa za kivinjari (kama vile IndexedDB, WebAssembly, na Cookies) ili kuboresha matumizi yako na kuongeza kasi ya mfumo. Teknolojia hizi hutuwezesha kuhifadhi nakala za muda za kazi zako (drafts) moja kwa moja kwenye kifaa chako, jambo linalokuhakikishia usalama na faragha ya hali ya juu kwa sababu data hizi hazisafiri kwenda kwenye seva zetu.